• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mimea "ikinyonya siki" itapata uwezo mkubwa zaidi wa kukinga ukame

    (GMT+08:00) 2017-07-03 16:01:50

    Utafiti mpya wa Japan unaonesha kuwa kuweka asidi ya acetic ambayo ni kemikali muhimu ya siki kwenye udongo kutainua uwezo wa mimea wa kukabiliana na ukame. Utafiti huo unatazamiwa kuvumbua teknolojia mpya ya kuisaidia mimea kukinga ukame kwa njia rahisi zaidi.

    Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, ukame umekuwa tatizo kubwa linalosababisha kupungua kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo duniani. Wazo muhimu la kutatua tatizo hilo ni kuongeza uwezo wa mimea kwa teknolojia ya kurekebisha jeni. Lakini matumizi ya teknolojia hii yanahitaji muda mrefu na gharama kubwa, hivyo watafiti wamekuwa wanatafuta njia nyingine rahisi zaidi.

    Watafiti wa Taasisi ya RIKEN ya Japan wakishirikiana na watafiti wa Chuo Kikuu cha Tokyo, wamefanya majaribio kwenye mimea aina ya Arabidopsis. Baada ya kuvuta asidi ya acetic iliyowekwa kwenye udongo, mimea hiyo ilianza kuzalisha asidi ya jasmonic, na asidi hiyo ikaweza kuihimiza jeni ya kukinga ukame kufanya kazi zaidi. Watafiti wamejaribu kutia asidi nyingine kwenye udongo, lakini zote hazikufanya kazi.

    Watafiti wamethibitisha kuwa asidi ya acetic pia inafanya kazi kwenye mazao mbalimbali yakiwemo mpunga, mahindi na ngano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako