• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza nguvu ya doria katika eneo la bahari ya visiwa vya Xisha kutokana na tishio la Marekani

    (GMT+08:00) 2017-07-03 18:28:07

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Bw. Wu Qian amesema kitendo cha manowari ya Marekani kuingia kwenye eneo la bahari ya visiwa vya Xisha vya China bila ruhusa, ni uchokozi unaokwenda kinyume kabisa na sheria, na China inapinga kithabiti kitendo hicho.

    Amesema Jeshi la China litaimarisha uwezo mbalimbali wa ulinzi, kuongeza nguvu ya doria baharini na angani kwa mujibu wa kiwango cha tishio ili kulinda mamlaka na usalama wa taifa.

    Tarehe 2 Julai manowari ya Stethem ya Marekani iliingia kwenye eneo la bahari ya visiwa vya Xisha bila ruhusa ya serikali ya China. Manowari za Luoyang, Suqian na Taishan za jeshi la majini la China na ndege mbili za kijeshi zilichukua hatua mara moja kuionya na kuifukuza manowari ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako