• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China azungumza na mwenzake wa Marekani Donald Tump kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2017-07-03 18:33:24

    Rais Xi Jinping wa China amebadilishana maoni na mwenzake wa Marekani Donald Trump kwa njia ya simu kuhusu uhusiano kati ya nchi zao na mkutano ujao wa viongozi wa kundi nchi za G20 utakaofanyika mjini Hamburg.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China imeeleza msimamo wake kwa Marekani na kutarajia Marekani itafuata kanuni ya China Moja na nyaraka tatu zinazohusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kushughulikia suala la Taiwan kwa njia inayofaa. Pia amesema pande mbili zinapaswa kushikilia kanuni ya kuheshimiana na kunufaishana, kuzingatia ushirikiano na kudhibiti tofauti zilizopo ili kusukuma mbele uhusiano huo.

    Rais Donald Trump amesema, uhusiano kati ya China na Marekani una mustakabali mzuri. Serikali ya Marekani inapenda kuendelea kutekeleza sera ya China Moja. Pia anatarajia kuzungumza na rais Xi na viongozi wengine kwenye mkutano ujao wa kundi la nchi za G20 kuhusu masuala yanayofuatilia zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako