• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sehemu ya mashariki mwa Libya yakumbwa na kukatika umeme

    (GMT+08:00) 2017-07-03 18:51:20

    Eneo lote la mashariki mwa Libya limekumbwa na kukatika kwa umeme kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa umeme.

    Taarifa iliyotolewa na shirika la umeme la Libya imesema vituo vyote vya Mashariki vimeharibika na kusababisha eneo lote la mashariki mwa Libya hadi Tobruk kukosa umeme. Shirika hilo limetoa mwito kwa wakazi wa huko kupunguza matumizi ya umeme ili kazi ya kufanya marekebisho ifanyike haraka.

    Shirika hilo lilitangaza ijumaa iliyopita kuwa sehemu za kusini na magharibi zilikumbwa na kukatika kwa umeme kutokana na mitambo kuharibiwa na joto kali.

    Kwa ujumla Libya inazalisha megawati elfu 5 kwa siku, ikiwa na upungufu wa megawati 1400, hasa kutokana na ongezeko la joto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako