• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi Tanzania unakua kwa kasi barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-07-03 19:26:51

    BALOZI mdogo wa Ujerumani nchini, John Reyes amesema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayokua kwa kasi kiuchumi katika Bara la Afrika hivyo kuvutia wawekezaji wengi kutokana na mazingira mazuri ya biashara.

    Akizungumza nyumbani kwake jana katika hafla ya kupongeza kampuni zinazotangaza bidhaa za Kijerumani katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba, Balozi Reyes amesema nchi yake inatazamia kuwekeza zaidi katika ardhi ya Tanzania.

    Katika Afrika Mahsariki na Kati pamoja na Afrika nzima Tanzania imeonesha kukua kwa kasi.

    Aidha amesema Kuna fursa nyingi za uwekezaji na ndiyo maana bidhaa kutoka Ujerumani zimekuwa zikiongezeka.

    Hivyo amesema atatumia nafasi yake kuhakikisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, kuwa na uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025, inatimia kwa kiasi kikubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako