• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania Bandari Dar kuongeza biashara, ya ndani na ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2017-07-03 19:27:24

    BANDARI ya Dar es Salaam ambayo ndio lango kuu la biashara nchini, inatarajia kuongeza uwezo wake wa kupokea meli kubwa na mizigo kutoka tani za sasa milioni 18 hadi kufikia milioni 28 ndani ya miaka saba ijayo.

    Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DSMGP), uliozinduliwa rasmi jana na Rais John Magufuli unatarajiwa kuongeza uchumi kwa kiwango kikubwa na uwezo wa bandari ya Dar es Salaam.

    Mradi huo unatarajiwa kuongeza biashara, ya ndani na ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na mikoa ya Afrika Kusini ya Maendeleo (SADC).

    Serikali, kupitia Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA), imeweka dola milioni 63 na Uingereza imetoa ruzuku ya dola milioni 12 kwa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID).

    Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedit Kakoko amesema mradi huo ukikamilika miezi 28 ijayo, itakuwa imeongeza uwezo wa kuhudumia shehena kutoka tani milioni 14 za sasa hadi tani milioni 28 ifikapo mwaka 2022 badala ya tani milioni 18 ambazo zingekuwa kikomo cha bandari ya sasa kama isipoendelezwa zaidi.

    Alafu itakuwa na uwezo wakupitisha meli kubwa zenye urefu wa zaidi ya mita 300 tofauti na sasa ambako meli zinazohudumiwa ni zile zenye urefu wa mita 240.

    Rais Magufuli amesema mradi huu utakaoagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 481 na itakuwa ina mchango mkubwa wa maendeleo ya ustawi wa Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako