• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Idadi ya barua zinazotumwa kupitia posta imeshuka kwa asilimia 50

    (GMT+08:00) 2017-07-03 19:27:52

    Idadi ya barua zinazotumwa na Wakenya kwa njia ya posta zimepungua kwa karibu nusu katika robo ya kwanza mwaka huu, ambayo imechangia kushuka kwa sekta ya posta nchini.

    Kulingana na takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano mwishoni mwa wiki iliyopita, Wakenya walituma barua milioni 8.2 katika miezi mitatu hadi Machi, asilimia 48.3 chini kuliko milioni 15.9 katika robo ya awali.

    Mwelekeo huu umeitaka serikali kutafuta njia vyanzo mbadala vya mapato katika sekta hiyo ili kuokoa Shirika la posta nchini Kenya.

    Barua zinazoingia za kimataifa zilishuka kwa asilimia 58 kwa kila robo ya mwaka hadi 964,013 wakati barua zinazosafiri zilipungua kwa asilimia 52.1 hadi 912,825.

    Takwimu hizi ni chini ya nusu ya zile ziliripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako