• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi vya Iraq vyaikaribia ngome ya IS ya Mosul

    (GMT+08:00) 2017-07-04 08:57:09

    Vikosi vya Iraq vimekomboa maeneo mapya kwenye ngome iliyobaki ya kundi la IS katika mji mkongwe wa Mosul baada ya mapambano makali yaliyosababisha vifo vya wapiganaji 67 wa kundi la IS.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Iraq vikosi hivyo vilikomboa maeneo ya Khatoniyah, Tuwalib na Ra's al-Kour na kufanikiwa kutegua mabomu 72 yaliyotegwa kando ya barabara. Aidha vikosi vilifungua njia kadhaa salama kwenye eneo linalokaliwa na watu wengi na kuweza kuwahamisha takriban raia 961.

    Kikosi cha kupambana na ugaidi, jeshi, Polisi na vikosi vya mwitikio wa haraka vinaendelea na mapambano ndani ya mji mkongwe, hata hivyo wanasonga mbele taratibu kutokana na upinzani mkali kutoka kwa wapiganaji wa kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako