• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini kuhimiza maslahi ya Afrika katika mkutano wa kilele wa G20

    (GMT+08:00) 2017-07-04 09:27:02

    Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema Afrika Kusini itahimiza na kuimarisha maslahi yake na ya Afrika katika mkutano ujao wa kilele wa kundi la nchi 20.

    Rais Zuma amesema msimamo huo unatokana na uelewa kwamba, kama kundi la G20 likisimamiwa vizuri linakuwa na fursa nzuri za kuhimiza mageuzi yanaohitajika ya utawala na kuelekeza ajenda ya maendeleo ya kimataifa.

    Msemaji wa Rais wa Afrika Kusini Bw Bongani Ngqulunga, amesema moja ya malengo makuu ya Afrika Kusini kwenye mkutano huo, ni kuanzisha sera ya kiuchumi na kimataifa itakayokuwa na matokeo mazuri kwa Afrika Kusini, Afrika na nchi zinazoendelea.

    Rais Zuma atahudhuria mkutano wa viongozi wa kundi la nchi 20 utakaofanyika wikiendi hii nchini Ujerumani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako