• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 700 wa kundi la Boko Haram wajisalimisha Nigeria

    (GMT+08:00) 2017-07-04 09:27:23
    Jeshi la Nigeria limesema wapiganaji 700 wa kundi la Boko Haram kwenye jimbo la Borno wamejisalimisha kwa jeshi la Nigeria.

    Mnadhimu mkuu wa jeshi la Nigeria Bw Tukur Buratai amesema katika maonesho ya kuadhimisha siku ya jeshi la Nigeria, kwamba jeshi hilo limepata mafanikio makubwa katika operesheni ya kupambana na kundi la Boko haram.

    Kundi la Boko Haram limesababisha mauaji ya watu zaidi ya elfu 20, na kufanya wengine milioni 2.3 kuwa wakimbizi tangu mwaka 2009.

    Mpaka sasa watuhumiwa 1,400 wa kundi hilo wanashikiliwa kwenye maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako