• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Syria latangaza kusimamisha vita kwa siku nne kwenye sehemu ya kusini

    (GMT+08:00) 2017-07-04 09:56:53

    Jeshi la Syria limetangaza kusimamisha vita kwa muda wa siku nne kwenye sehemu ya kusini kuanzia tarehe 2 mwezi huu.

    Taarifa iliyotolewa na jeshi la Syria imesema usitishaji vita unatekelezwa kwenye mikoa ya kusini ya Dara'a, AlQunaytirah na Al Suwayda, ili kuunga mkono mchakato wa amani na maafikiano ya kitaifa. Taarifa imesisitiza kuwa jeshi la Syria litajibu kitendo chochote cha kuvuruga usimamishwaji wa vita.

    Hii ni mara nyingine kwa jeshi la Syria kutangaza kusimamisha vita baada ya kusitisha vita kwa saa 48 tarehe 17 mwezi uliopita.

    Duru ya tano ya mazungumzo ya amani kuhusu suala ya Syria itafanyika leo na kesho mjini Astana, Kazakhstan. Habari zinasema kusimamisha vita kuna lengo la kupunguza hali ya wasiwasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako