• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje ya Qatar awasili Kuwait na kuwasilisha majibu ya Qatar kwa nchi nne

    (GMT+08:00) 2017-07-04 09:57:15

    Waziri wa mambo ya nje wa Qatar amewasili Kuwait na kuwasilisha majibu ya Qatar kwa Saudi Arabia, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain, ambazo zilitoa taarifa ya pamoja ya kuipatia Qatar saa 48 zaidi kutoa majibu yake kuhusu orodha ya matakwa 13 ya nchi hizo.

    Habari zinasema waziri wa mambo ya nje wa Qatar Bw Mohammed Al-Thani atawasilisha barua ya Mfalme Al Thani wa Qatari kwa Mfalme Al-Sabah wa Kuwait, ikiwa na majibu rasmi ya Qatar kwa matakwa 13 ya nchi hizo nne. Kuwait itawasilisha majibu hayo ya Qatar kwa nchi nyingine.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Misri imesema mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Bahrain, Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia watakutana kesho mjini Cairo kujadili suala la Qatar. Misri imesema nchi hizo zitaratibu misimamo yao kwa mujibu wa hatua zitakazochukuliwa kwa Qatar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako