• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya waonya kuhusu uwezekano wa kutokea vurugu wakati wa uchaguzi nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-07-04 10:05:13

    Umoja wa Ulaya umeonya kuwa vurugu zinaweza kutokea nchini Kenya kama mchakato wa uchaguzi ukishindwa kuepusha udanganyifu kama vile kudhibiti uchaguzi na kuwatishia wapiga kura.

    Mwangalizi mkuu wa ujumbe wa uangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya Bibi Marietje Schaake amesema, kama hatua imara za kukabiliana na hali hiyo hazitachukuliwa vurugu zinaweza kutokea.

    Bibi Schaake amesema hayo kwenye uzinduzi wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Kenya utakaofanyika mwezi Agosti.

    Pia ameeleza wakenya wengi zaidi wameonesha wasiwasi kuhusu uwezekano wa kutokea vurugu wakati na baada ya uchaguzi, lakini amesisitiza kuwa hali hiyo inaweza kuepukika kama wagombea wanaweza kufanya mazungumzo badala ya migongano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako