• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la vijana la Mkutano wa Kamati ya Urithi wa Dunia laitaka jumuiya ya kimataifa kuhifadhi urithi

    (GMT+08:00) 2017-07-04 18:29:26

    Kongamano la vijana la Mkutano wa 41 wa Kamati ya Urithi wa Dunia ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limetoa taarifa likiitaka jumuiya ya kimataifa kuimarisha uhifadhi na utengenezaji wa urithi wa kiutamaduni na kimaumbile.

    Vijana 32 kutoka nchi 32 waliohudhuria kongamano hilo wanaoshughulikia uhifadhi wa mabaki ya kihistoria wameeleza wasiwasi wao kuhusu uharibifu wa maeneo ya urithi, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi zote kuhifadhi mabaki ya kihistoria na kufuatilia maendeleo endelevu ya kijamii.

    Mkutano wa 41 wa Kamati ya Urithi wa Dunia ulifunguliwa jumapili mjini Kracow, Poland, na utajadili maombi 34 ya maeneo ya kuwekwa kwenye orotha ya urithi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako