• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini yafanya jaribio la kurusha makombora ya masafa marefu katika bahari ya mashariki nchini humo

    (GMT+08:00) 2017-07-04 18:32:22

    Korea Kaskazini imetangaza kuwa imefanikiwa katika jaribio la kurusha kombora la masafa marefu, na kusema hiyo ni hatua kubwa katika maendeleo ya mradi wa kutengeneza makombora.

    Jaribio hilo ni hatua muhimu ya mpango wenye utata wa kutengeneza makombora wa Korea Kaskazini, ambayo unalenga kuhakikisha ulinzi wa usalam wa nchi na haki ya uwepo wa taifa hilo dhidi ya vitisho kutoka Marekani.

    Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang alipozungumzia suala hilo amesema China inapinga Korea Kaskazini kurusha makombora kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako