• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kusukuma mbele utatuzi wa masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati

    (GMT+08:00) 2017-07-04 18:41:25

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China itatekeleza wajibu wake kwa makini baada ya kuwa mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kusukuma mbele utatuzi wa maswala ya Afrika na Mashariki ya Kati kwa kufanya mikutano na mijadala mbalimbali.

    Geng Shuang amesema, mwezi huu Baraza hilo litafanya mikutano karibu 30 kujadili masuala ya Mashariki ya Kati ikiwemo Syria, Yemen, Iraq na Lebanon, na masuala ya Afrika ikiwemo Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na ofisi ya Umoja wa Mataifa kanda Afrika Magharibi na kanda ya Sahel, pia litafanya mijadala miwili kufuatilia ujenzi wa uwezo wa kulinda amani na usalama barani Afrika na suala la Palestina na Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako