• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara kati ya China na Russia yaongezeka kwa utulivu

    (GMT+08:00) 2017-07-04 20:25:46

    Tangu miaka kadhaa iliyopita, uchumi wa dunia umekuwa unafufuka polepole. Lakini biashara kati ya China na Russia imeongezeka kwa utulivu. Wataalamu wamesema, China na Russia zimesaidiana kiuchumi, na katika siku za baadaye nchi hizo mbili zitaimarisha zaidi ushirikiano kwa njia ya jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai na mfumo wa nchi za BRICS, na kupanua biashara kati yao.

    Takwimu zilizotolewa na idara kuu ya forodha ya China zinaonesha kuwa, mwaka 2016 thamani ya biashara kati ya China na Russia imeongezeka kwa asilimia 2.2. katika miezi mitano ya kwanza mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na Russia imefikia yuan bilioni 223.1, na kuongezeka kwa asilimia 33.7 kuliko mwaka 2016 wakati kama huu. Naibu mkurugenzi wa taasisi ya soko la kimataifa ya wizara ya biashara ya China Bw. Bai Ming, ameona China na Russia bado zina fursa kubwa kwenye kusaidiana kiuchumi.

    Kabla ya maonesho ya nne ya bidhaa za China na Russia yaliyofanyika mwezi uliopita, naibu waziri wa maendeleo ya uchumi wa Russia aliwahi kusema, bidhaa zilizouzwa na Russia kwa China zinaongezeka, bidhaa hizo si kama tu ni mafuta na madini, bali pia ni mashine na mazao ya kilimo. Alikadiria kuwa kwa mujibu wa mwendo wa hivi sasa, thamani ya biashara kati ya China na Russia mwaka huu inakadiriwa kufikia dola za kimarekani bilioni 80.

    Hivi sasa hali ya jumla ya uchumi nchini Russia ni tulivu. Thamani ya jumla ya uzalishaji nchini Russia imeongezeka kwa miezi mitatu mfululizo, hii imeonesha kufufuka kwa uchumi wa Russia kumeingia kwenye kipindi kipya. Wachambuzi wameona kuwa China na Russia zitakuwa na fursa nyingi zaidi katika njia za kukuza biashara.

    Bw. Bai Ming amesema katika miaka ya karibuni iliyopita, China imerekebisha miundo ya uchumi, na kubadilisha njia ya kukuza biashara kwa nje, bidhaa nyingi za China zenye sifa nzuri zinakaribishwa na warussia. Wakati huo huo, biashara ya elektroniki nchini China inaendelezwa kwa kasi, wateja wengi wa Russia wanapenda kununua bidhaa za China kwa njia ya biashara ya elektroniki.

    Bw. Bai pia amesema mfumo wa ushirikiano wa kimataifa pia umetoa fursa zaidi kwa biashara kati ya China na Russia. Katika siku za baadaye, nchi hizo mbili zitatumia fursa hizo ili kuhimiza maendeleo ya biashara kati yao. Amesema jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai imeufanya uhusiano kati ya China na Russia uwe karibu zaidi. Mkutano wa tisa wa viongozi wa nchi za BRICS utafanyika mwaka huu huko Xiamen nchini China, na kuleta fursa nyingi zaidi. Ameongeza kuwa maendeleo ya uchumi na biashara kati ya China na Russia, si kama tu ni ongezeko la biashara, bali pia ni hali ya kusaidiana kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, na hadhi zao kwenye utandawazi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako