• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Benki ya Barclays kufunga matawi 7

    (GMT+08:00) 2017-07-04 20:32:26

    Benki ya Barclays imetangaza mpango wa kufunga matawi 7 nchini Kenya katika hatua ya kustawisha harakati za biashara.

    Katika taarifa kwa vyombo vya habari,benki hiyo itafunga vituo 2 vya Meru ,Wundanyi na mkoa wa pwani.

    Jijini Nairobi vituo vya benki hiyo vya Haile Selasie,Waiyaki,Kawangware na Rahimtulla vitasitisha shughuli zake na matawi ya Nakumatt Meru na Wundanyi pia yatafungwa.

    Wafanyikazi wanaohudumu katika matawi ya benki hizi wanatarajiwa kupewa majukumu mengine katika huduma za benki hiyo kwa mujibu wa usimamizi wa benki hiyo.

    Hatua hii inajiri siku chache baada ya benki hiyo kuwasimamisha wafanyikazi 130 kufuatia ukosefu wa fedha .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako