• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Russia

    (GMT+08:00) 2017-07-04 20:44:26

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na waziri mkuu wa Russia Bw. Dmitry Medvedev mjini Moscow, Russia..

    Katika mazungumzo yao, Bw. Medevedv amesema uhusiano kati ya nchi hizo mbili uko katika kipindi kizuri, na ushirikiano wa wenzi wa kimkakati unaendana na maslahi ya watu wao na unasaidia amani na maendeleo ya dunia

    Kwa upande wake, Rais Xi amesema pande hizo mbili zitapanua ushirikiano katika sekta za uchumi, biashara, uwekezaji na nishati, kutekeleza miradi mikubwa ya utengenezaji, na kuanzisha mapema mradi wa reli ya kasi kati ya Mocow na Kazan. Pia kuhimiza ushirikiano unaovuka mpaka katika ujenzi wa miundo mbinu, uendelezaji wa rasilimali, kilimo cha kisasa na uzalishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako