• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya uchaguzi yaundwa upya, mchakato kuendelea bila Malinzi.

    (GMT+08:00) 2017-07-05 09:02:22

    Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko ya kamati ya uchaguzi na kuwaengua wajumbe wanne walioonyesha kumtetea Rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi ambaye kwa sasa yuko rumande kwa tuhuma mbalimbali.

    Uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha kamati ya utendaji ya TFF kilichofanyika jana mchana makao makuu ya shirikisho hilo, uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam chini ya kaimu Rais, Wallace Karia.

    Uchaguzi wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako