• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Iraq latangaza kuukomboa Mosul ndani ya siku mbili

    (GMT+08:00) 2017-07-05 09:28:42

    Jeshi la Iraq limetangaza kuwa litaukomboa mji wa Mosul ndani ya siku mbili.

    Kamanda wa kituo cha uongozi wa operesheni za kijeshi mkoani Nineveh Bw al-Juburi amesema mji wa Mosul utakuwa umekombolewa kabla ya terehe 6 mwezi huu. Hivi sasa ni eneo la Maydan tu mjini Mosul bado halijakombolewa. Kukombolewa kwa eneo hilo kutamaanisha kuwa mji mzima wa Mosul umekombolewa.

    Jeshi la Iraq lilianza mashambulizi magharibi mwa mji wa Mosul tangu tarehe 18 mwezi uliopita, ambako ni medani ya mwisho ya vita ya kuukomboa mji wa Mosul.

    Bw al-Juburi ameongeza kuwa baada ya kuukomboa mji huo, jehsi la Iraq litahamia Tal Afar, ambayo ni ngome ya mwisho ya Kundi la IS mkoani Nineveh.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako