• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Russia zatoa taarifa ya pamoja kuhusu suala la peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-07-05 09:32:19

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Russia Sergei Lavrov jana huko Moscow wamesaini taarifa ya pamoja kuhusu suala la Peninsula ya Korea.

    Kwenye taarifa hiyo China na Russia zinaona hatua ya Korea Kaskazini inakwenda kinyume na maazimio husika ya Baraza la usalama wa Umoja wa Mataifa, hazikukubaliani hatua hiyo, na kuitaka Korea Kaskazini ifuate kwa makini maazimio ya Baraza la usalama.

    Taarifa pia inasema China na Russia zinafuatilia maendeleo ya hali ya peninsuala ya Korea na sehemu za karibu, zinapinga vitendo na kauli yoyote zitakazochochea mgogoro, kuzitaka nchi husika zijizuie na kuepusha hatua za uchokozi, kuonyesha nia ya kufanya mazungumzo bila masharti, na kufanya juhudi kupunguza hali ya wasiwasi ya kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako