• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yawalaumu waasi kwa kuleta hali ya wasiwasi kwenye eneo la mpaka

    (GMT+08:00) 2017-07-05 09:49:25

    Jeshi la Sudan Kusini limewalaumu waasi kwa kusababisha hali ya kukosekana kwa usalama kwenye eneo la mpaka na Uganda, lenye wakimbizi zaidi ya milioni 1.

    Msemaji wa jeshi la ukombozi la Sudan Kusini SPLA Bw. Domic Chol amesema hayo mjini Juba baada ya kuripotiwa kuwa baadhi ya makundi yenye silaha yanawateka wakimbizi na kupora ng'ombe kwenye kambi za wakimbizi za katika wilaya ya Moyo nchini Uganda.

    Amesema hao ni waasi wa Sudan Kusini, wanaovaa sare na kuonekana kama wapiganaji wa jeshi la serikali. Amesema kama hawatachukuliwa hatua basi watakuwa tishio kwa nchi za jirani.

    Matukio haya yameongeza wasiwasi miongoni mwa wakimbizi na kufanya idara za usalama nchini Uganda kuwa na tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea kwa vurugu kwenye eneo la mpaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako