• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa umoja wa mataifa alaani jaribio la makombora la Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-07-05 09:49:51

    Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Bw Antonio Guterres amelaani vikali jaribio la kombora la masafa marefu lililofanywa jana na Korea kaskazini.

    Bw Guterres amesema hili ni tukio lingine la Korea Kaskazini la ukiukaji wa maazimio ya baraza la usalama la umoja wa mataifa na linaongeza hali ya wasiwasi. Ameutaka uongozi wa Korea Kaskazini kuacha vitendo vya uchokozi na kutekeleza kikamilifu matakwa ya jumuiya ya kimataifa.

    Pia ameeleza umuhimu wa jumuiya ya kimataifa kuwa na umoja katika kukabiliana na changamoto hiyo.

    Jana Korea Kaskazini ilitangaza kuwa imefanikiwa kufanya jaribio la kombora la masafa marefu, na kulitaja kuwa ni hatua ya mwisho ya kukamilisha nguvu ya nyuklia ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako