• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yasimamisha utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini

    (GMT+08:00) 2017-07-05 10:05:42

    Rais John Magufuli wa Tanzania amesimamisha utoaji leseni mpya za uchimbaji wa madini kwa wawekezaji.

    Akiongea katika siku ya pili ya ziara yake kwenye kanda ya ziwa, Rais Magufuli pia ameiamuru wizara ya nishati na madini kuhakikisha inasimamisha mara moja utoaji leseni za uchimbaji madini.

    Amesema leseni zote za uchimbaji wa madini zilizotolewa na serikali zinatakiwa kukaguliwa upya ili kujua jinsi serikali inavyonufaika.

    Rais Magufuli amesema, madini ikiwemo dhahabu ambazo zinazochimbwa nchini humo zinamilikiwa na watanzania, na serikali yake haitavumilia kuona baadhi ya watu wananufaika na maliasili za nchi wakati walio wengi wanaishi maisha duni.

    Wiki iliyopita, serikali ilijadili mswada wa sheria kuhusu kukagua na kurekebisha sheria za madini kufuatia amri iliyotolewa hivi karibuni na rais huyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako