• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapitia mtaala wa elimu wakati ikipambana na msimamo mkali

    (GMT+08:00) 2017-07-05 10:06:30

    Wizara ya elimu ya Kenya imeharakisha ukaguzi wa mtaala wa elimu kuhakikisha shule zinafundisha uzalendo na uvumilivu miongoni mwa wanafunzi, ili kuwaepusha kuchochewa na msimamo mkali.

    Waziri wa elimu wa Kenya Bw. Fred Matiangi amesema, mtaala wa elumi uliorekebishwa ni muhimu katika kuimarisha mapambano dhidi ya msimamo mkali wa kimabavu ambao unaenea haraka katika sehemu za pembezoni nchini humo.

    Amesema, ongezeko la msimamo mkali na matumizi ya mabavu linatishia utulivu na maendeleo ya nchi hiyo, kwa hiyo mfumo wa elimu unatakiwa kutoa mafunzo kwa vijana ili waweze kuhimiza amani katika familia, jamii na nchi nzima.

    Pia amesema, jumuiya ya kimataifa imekubaliana kutumia nguvu ya shule za elimu kupambana na msimamo mkali, na imepata maendeleo katika sehemu maskini zilizoachwa nyuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako