• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China awasili Berlin kwa ziara rasmi

    (GMT+08:00) 2017-07-05 10:19:53

    Rais Xi Jinping wa China amewasili Berlin na kuanza ziara yake rasmi nchini Ujerumani, baada ya kukamilisha ziara yake nchini Russia.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, uhusiano kati ya China na Ujerumani una fursa mpya ya maendeleo. Pia amesema China inapenda kushirikiana na Ujerumani kufanikisha mkutano wa kilele wa G20 utakaofanyika mjini Hamburg, kwenye msingi wa mafanikio yaliyopatikana katika mkutano wa kundi hilo uliofanyika mwaka jana mjini Hangzhou.

    Kwenye ziara yake nchini Russia, marais wa China na Russia walisaini taarifa ya pamoja kuhusu uhusiano kati ya nchi zao. Taarifa hiyo inasema, China na Russia zitajitahidi kuimarisha ushirikiano wa kiusalama, maingiliano ya kiutamaduni na uratibu kati ya pande mbili kwenye masuala ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako