• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chansela wa Ujerumana akutana na Rais wa China

    (GMT+08:00) 2017-07-05 18:43:53

    Chansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel amekutana na Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini humo katika makazi ya zamani ya Max Libermann mjini Berlin, Ujerumani.

    Katika mazungumzo yao Bibi Merkel amesema, hivi sasa, uhusiano kati ya China na Ujerumani unaendeleza vizuri, na mafanikio makubwa yamepatikana katika ushirikiano wa sekta mbalimbali. Amesema Ujerumani inazingatia mchango uliotolewa na China katika masuala ya kimataifa na kuishukuru China kwa kuiunga mkono Ujerumani kufanikiwa kufungua mkutano wa G20 mjini Hamburg.

    Kwa upande wake, Rais Xi amesema, mafanikio makubwa yamepatikana katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ujerumani tangu mazungumzo yao yaliyofanyika Hangzhou mwaka jana, na kuwa ziara hiyo itasukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili. Pia amesema anatarajia Ujerumani kutoa mchango kusukuma mbele uhusiano huo, kudumisha maendeleo ya kiwango cha juu, na kuuhimiza utandawazi wa kiuchumi wa dunia kunufaisha zaidi nchi mbalimbali.

    Rais Xi amesema China inaikaribisha Ujerumani kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako