• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa Al Shabaab wavamia kituo cha polisi nchini Kenya na kuharibu mawasiliano

    (GMT+08:00) 2017-07-05 17:44:29

    Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab la Somalia wamevamia kituo cha polisi katika mji wa pwani wa Lamu kaskazini mwa Kenya leo asubuhi na kuharibu mnara wa mawasiliano katika eneo hilo.

    Kamishna wa Kaunti ya Lamu Joseph Kanyiri amethibitisha tukio hilo, na kusema wapiganaji hao walivamia kijiji kimoja kwenye kaunti hiyo na kuharibu mnara wa simu wa kampuni ya Safaricom, hivyo kuvuruga mawasiliano katika eneo hilo.

    Kamanda wa polisi kanda ya pwani Philip Tuimur amesema, vikosi vya usalama viliwasili haraka kwenye eneo la tukio na kukabiliana na washambuliaji hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako