• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi wa China nchini Ghana wafanya kongamano la uhusiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2017-07-05 18:06:33

    Ubalozi wa China nchini Ghana na taasisi ya utawala wa kidemokrasia ya Ghana kwa pamoja zimefanya kongamano kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika huko Acra, mji mkuu wa Ghana.

    Kongamano hilo limehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 100 wakiwemo wataalamu, wanaviwanda na wafanyabiashara kutoka China, Ghana, Zimbabwe na Cote d'Ivoire.

    Kwenye kongamano hilo, makamu wa rais wa Ghana Bw. Mahamudu Bawumia amesema China ni mwenzi muhimu zaidi wa ushirikiano wa Afrika. Amesema kwa kuwa hivi sasa nchi za Afrika zinatilia maanani ujenzi wa miundo mbinu na mageuzi ya viwanda na kilimo, zitatafuta njia mpya ya ushirikiano na China, ili kuongeza uwekezaji na kupata mafanikio kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako