• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran na Russia kushirikiana kuizuia Marekani isiingilie mambo ya Syria

    (GMT+08:00) 2017-07-05 18:06:51

    Katibu wa kamati kuu ya usalama wa taifa nchini Iran Bw. Ali Shamkhani na katibu wa kamati ya usalama wa taifa ya Russia Bw. Nikolai Patrushev wamezungumza kwa njia ya simu na kusema pande hizo mbili zitaimarisha ushirikiano katika mambo ya Syria ili kuzuia Marekani isiingilie mambo ya nchi hiyo kwa njia haramu.

    Bw. Shamkhani amesema visingizio na hatua za Marekani za kuingilia suala la Syria zitazidisha mgogoro na kusaidia kuimarisha nguvu za kigaidi katika kanda, hivyo ni muhimu kuimarisha ushirikiano kati ya Iran na Russia ili kuzuia hatua za Marekani.

    Bw. Patrushev amesema kutokana na juhudi za pamoja za Russia na Iran, Syiria imepata maendeleo ya kuridhisha katika mchakato wa kisiasa na kivita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako