• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 5 wa mawaziri wa elimu wa nchi za BRICS wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2017-07-05 18:49:03

    Mkutano wa 5 wa mawaziri wa elimu wa nchi za BRICS wenye lengo la kuhimiza maendeleo na haki, umefanyika hapa Beijing.

    Washiriki wa mkutano huo wamesaini azimio la elimu la Beijing ambalo linaeleza ushirikiano wa elimu wa nchi hizo katika siku za baadaye. Azimio hilo limesema, nchi za BRICS zitaendelea kuunga mkono mtandao wa ushirikiano wa elimu, sayansi na uvumbuzi kati ya nchi wanachama wa BRICS. Pia zitahimiza vyuo vikuu vya nchi hizo kushiriki kwenye jumuiya ya vyuo vikuu ya nchi za BRICS, kuongeza ushirikiano wa kiutamaduni kwa kutumia lugha mbalimbali katika elimu ili kuongeza maelewano ya kihistoria na kiutamaduni kati yao.

    Waziri wa elimu wa China Chen Baosheng amesema, azimio hilo limeonyesha kwamba, ushirikiano wa elimu kati ya nchi za BRICS umeanza kufunika elimu ya juu na pia elimu ya msingi. Pia umeongezeka kutoka ushirikiano wa elimu hadi ushirikiano wa uvumbizi wa sayansi, kubadilishana habari na mawasiliano ya utamaduni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako