• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • India kuingia kwenye ardhi ya China kwa njia haramu ni kinyume na kanuni za uhusiano wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-07-05 18:50:01

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Geng Shuang amesema kitendo cha India cha kuingia kwenye ardhi ya China kwa njia haramu kimekwenda kinyume na kanuni za uhusiano wa kimataifa zinazopendekezwa na nchi hiyo.

    Geng amesema hayo baada ya taarifa za askari wa India kuingia katika ardhi ya China kwa njia haramu, na kusema ni lazima India irudishe mara moja askari wote waliovuka mpaka ili hali isizidi kuwa mbaya.

    Amesema China inaitaka India kusahihisha kosa lake kwa hatua halisi, kuonesha udhati wa kutatua suala la mpaka na kuendeleza uhusiano kati ya nchi mbili, na kuweka mazingira mazuri kwa maendeleo ya kawaida ya uhusiano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako