• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa maji Mpwapwa wakamilika

    (GMT+08:00) 2017-07-05 19:39:34

    MRADI wa maji uliokuwa unajengwa katika kijiji cha Wiyenzele kata ya Chipogolo umekamilika na unatarajia kuwanufaisha wakazi 3,164.

    Kukamilika kwa mradi huo, kutaongeza ukuaji wa uchumi wa kijiji hicho.

    Mradi huo uliogharimu jumla ya zaidi ya shilingi milioni 3.4 na una uwezo wa kuzalisha lita 90,000 kwa siku.

    Mmoja wa mwanakijiji Anna Chisaluni amesema kabla ya mradi huo kukamilika wakazi wa kijiji hicho walikuwa wanatembea umbali wa kilometa tatu hadi tano kwenda kuchota maji katika mabwawa ya kienyeji ambayo maji hayo hayakuwa safi na salama kwa maisha ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako