• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yasema magaidi 10 wa Al-Shabaab wauawa katika mashambulizi ya anga

    (GMT+08:00) 2017-07-06 09:26:58

    Serikali ya Somalia imethibitisha kuwa magaidi 10 wa kundi la Al-Shabaab waliuawa kwenye mashambulizi ya anga yaliyofanywa jumapili usiku na jeshi la Somalia na washirika wake. Kwa mujibu wa wizara ya habari, utamaduni na utalii, mashambulizi hayo yaliwalenga magaidi wa Al-Shabaab kwenye maeneo ya kaskazini ya Kismayu, kusini mwa Somalia. Taarifa hiyo imetolewa kufuatia jeshi la Marekani kuthibitisha jumatatu kuwa lilifanya shambulizi la anga dhidi ya kundi la Al-Shabaab nchini Somalia, wakati nchi hiyo inaimarisha mapambano dhidi ya kundi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako