• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Murray na Konta wazidi kupepeta Michuano ya tennis ya Wimbledon

    (GMT+08:00) 2017-07-06 09:34:19

    Michuano ya mchezo wa tennis ya Wimbledon iliendelea jana ambapo Muingereza Andy Murray alikuwa uwanjani katika raundi ya pili dhidi ya Dustin Brown raia wa Ujerumani.

    Katila mchezo huo Murray ameendeleza wimbi la ushindi baada ya kumshinda Dustin Brown kwa seti 6-3 6-2 6-3 katika mchezo ambao ulikuwa wa kuvutia sana.

    Dustin Brown alionekana angeweza kuleta upinzani mkubwa kwa Murray kama alivyofanya kwa Rafael Nadal mwaka juzi lakini mchezaji huyo namba moja wa tennis alitulia na kumzamisha Brown.

    Ukiachilia mbali Murray kuna Muingereza mwingine aliyekuwa uwanjani ambaye ni Johanna Konta aliyekuwa akipambana na Donna Vekic katika mchezo ambao Johanna aliibuka na ushindi wa seti 7-6 4-6 na 10-8 katika mchezo uliochukua saa tatu na dakika 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako