• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Alexandre Lacazette asajiliwa na Arsenal kwa mkataba wa miaka mitano

    (GMT+08:00) 2017-07-06 09:35:10

    Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alexandre Lacazette toka timu ya Lyon kwa dau la pauni Milioni 52.6 na kuvunja rekodi ya usajili ya timu hiyo.

    Usajili wa kiungo Mjerumani Mesut Ozil ndio ulikua wa bei ghali zaidi klabuni hapo aliposajiliwa mwaka 2013, akitokea Real Madrid kwa dau la pauni milioni 42.4.

    Lacazette amesaini mkataba wa miaka mitano kuwatumika washika bunduki hao wa London, mshambuliaji huyu atasafiri na timu wikiendi hii kuelekea Sydney kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki.

    Msimu uliopita, Lacazette alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Ufaransa alikozipasua nyavu mara 28 na ameshapiga jumla ya mabao 129 katika mechi 275 tangu alipoanza kuichezea timu ya kwanza msimu wa 2009/10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako