• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usajili: tetesi za usajili wa soka barani Ulaya kwa siku ya Jumatano

    (GMT+08:00) 2017-07-06 09:36:22

    Siku zinazidi kuhesabika kwa safari ya Everton kwenda nchini Tanzania, lakini tetesi mpya kutoka ndani ya klabu hiyo ni usajili wa Wayne Rooney ambapo inasemekana mshambuliaji huyo anaweza kusaini katika klabu ya Everton.

    Klabu ya soka ya Real Madrid imekamilisha usajili wa Theo Hernandez kutoka klabu ya Atletico Madrid kwa dau la €24m ambapo amesaini mkataba wa miaka 6.

    Baada ya kumsaini mshambuliaji wa Olympique Lyon Alexandre Lacazette, sasa klabu ya Arsenal imepiga hodi katika klabu ya Monaco kwa ajili ya kumnunua mlinzi Thomas Lemar.

    Inasemekana kocha wa Manchester United Jose Mourinho hana furaha na jinsi klabu hiyo inavyoendesha suala la usajili, Mourinho anawataka wachezaji kadhaa wakubwa lakini inaonekana kuchelewa.

    Baada ya kupoteza namba ya kudumu katika kikosi cha Real Madrid hatimaye mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Fabio Contrao amesaini kuichezea klabu ya Sporting CP kwa mkopo.

    Taarifa zinasema vilabu vya Chelsea na As Roma vimeshafanya makubaliano kuhusu uhamisho wa beki Antonio Rudiger ambapo atakwenda Chelsea kwa dau la €34m.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako