• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Kenya wako kwenye tahadhari kuepusha mapambano kabla ya uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2017-07-06 09:47:04

    Idara za usalama nchini Kenya ziko kwenye tahadhari ya hali ya juu ili kuepusha vurugu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini humo Agosti 8.

    Kamanda wa polisi wa Kenya Inspekta Jenerali Joseph Boinnet amewaambia wanahabari kuwa idara mbalimbali za usalama zimejipanga kuhakikisha zinalinda sheria na utaratibu wa jamii.

    Bw Boinnet amesema hayo wakati waangalizi wa Umoja wa Ulaya wameonyesha wasiwasi kuhusu uwezekano wa kutokea vurugu kwenye baadhi ya maeneo ya Kenya. Shirika la haki za binadamu lenye makao yake nchini Marekani Human Rights Watch, limesema hali ya mvutano inafukuta kwenye eneo la kaunti ya Naivasha.

    Habari pia zinasema polisi wameimarisha msako wa wapiganaji 200 wa kundi la Al-Shabaab waliovamia kambi ya polisi na kuwaua polisi watatu katika eneo la Lamu. Polisi mmoja mwingine haijulikani aliko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako