• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zambia atangaza hali ya dharura kutokana na vurugu zilizosababishwa uharibifu

    (GMT+08:00) 2017-07-06 09:48:05

    Rais Edgar Lungu wa Zambia jana alitangaza hali ya dharura kutokana na kuwepo kwa vitendo vya kuvunja sheria vinavyosababisha uharibifu wa mali za umma.

    Hatua hiyo inatokana na matukio yaliyotokea jumanne kwenye soko la wazi mjini Lusaka ambapo watu wasiojulikana walichoma soko hilo na kusababisha uharibifu mkubwa.

    Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni Rais Lungu amesema amechukua uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka anayopewa na katiba, ili kulinda amani, utulivu, na usalama wa taifa. Rais Lungu amekumbusha kuwa serikali imekuwa ikiwaasa watu mara kwa mara kuepuka vitendo vya kutowajibika na kueleza kusikitishwa na watu kutoitikia mwito huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako