• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa watoa mwito wa kuimarisha utalii wa ndani kwa kanda za Afrika

    (GMT+08:00) 2017-07-06 09:48:33

    Ripoti iliyotolewa na Umoja wa mataifa imewataka viongozi wa nchi za Afrika kuweka mkazo kwenye kuendeleza utalii wa kikanda na wa bara zima.

    Ripoti ya mwaka huu ya maendeleo ya uchumi barani Afrika, inasema utalii wa ndani barani Afrika unaongezeka na unatoa fursa ya uchumi na kuwa na vyanzo vingi vya biashara ya nje.

    Umoja wa mataifa umeutangaza mwaka 2017 kuwa mwaka wa utalii endelevu, na kusema barani Afrika watalii wanne kati ya watalii kumi wanatoka barani Afrika kwenyewe, na kwenye eneo la kusini mwa sahara idadi hiyo ni zaidi ikifika watalii wawili kati ya watatu.

    Katika muda wa miongo miwili iliyopita, kumekuwa na ongezeko kubwa la utalii barani Afrika na watalii kutoka nje wameongezeka kutoka asilimia 6 kwa mwaka hadi asilimia 9 kwa mwaka, kati ya mwaka 1995 na mwaka 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako