• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Messi kuendelea na Barcelona hadi 2021

    (GMT+08:00) 2017-07-06 10:02:09

    Mshambuliaji nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amekubali kutia saini mkataba mpya ambao utamuweka katika klabu hiyo hadi 2021. Awali Lionel Messi mwenye miaka 30 alikuwa kwenye mvutano na klabu yake kwa kukataa kuongeza mkataba mpya kutokana na kutofurahia baadhi ya mambo nchini Uhispania hususan masuala ya kodi ambayo yameitia doa historia yake ya soka kwa kuonekana mkwepa kodi.

    Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d'Or mara tano ambaye yupo kwenye Honey Money na mkewe Antonella Roccuzzo kwenye mkataba wake mpya atalipwa kiasi cha Euro Milioni 300 kwa miaka yote mine, na anatarajiwa kutia saini mkataba huo atakaporejea kushiriki mazoezi. Messi alijiunga na klabu ya Barca akiwa na miaka 13.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako