• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri wakutana Cairo

    (GMT+08:00) 2017-07-06 10:12:19

    Mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri wamekutana jana mjini Cairo kujadili majibu rasmi yaliyowasilishwa na Qatar kwa ajili ya kutatua mgogoro wa kidiplomasia na nchi hizo.

    Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo nne jana wametoa taarifa ya pamoja wakisema kwamba nchi hizo haziridhiki na majibu ya Qatar na kuyataja kuwa ni "mtizamo hasi na kutokuwa na mambo halisi". Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia amesema kuwa vikwazo dhidi ya Qatar vitaendelea.

    Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Qatar Bw Mohammed Al-Than amesema serikali ya Qatar itachukua hatua zote kuwalinda wananchi wake, pia amelaani kuwa kitendo cha kuizuia Qatar kimeharibu mamlaka ya nchi. Ameongeza kwamba serikali ya Qatar itaendelea na juhudi za kuondoa tofauti kupitia mazungumzo, lakini inapinga nchi za nje kuingilia mambo yake ya ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako