• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China na chansela wa Ujerumani wahudhuria uzinduzi wa jumba la Panda katika bustani ya wanyama ya Berlin

    (GMT+08:00) 2017-07-06 10:16:47

    Rais Xi Jinping wa China na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel jana walihudhuria uzinduzi wa jumba la Panda katika bustani ya wanyama ya Berlin.

    Rais Xi Jinping amesema ni muhimu kuanzisha tena ushirikiano kati ya China na Ujerumani kwenye utafiti wa uhifadhi wa panda wakati wa kuadhimisha miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo. Anatumai kuwa panda hao wawili watapunguza umbali kati ya nchi hizo mbili, na kuwa mabalozi wapya wa urafiki kati ya nchi hizo mbili.

    Viongozi hao pia wametazama mechi ya kirafiki ya soka kati ya vijana wa China na Ujerumani.

    Rais Xi amesema, ushirikiano kwenye mchezo wa soka kati ya China na Ujerumani unasonga mbele, na anaamini kuwa ushirikano huo utakuwa na manufaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako