Reli ya SGR ya Kenya inatarajiwa kupunguza hasara za mizigo kwa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki wanaoingiza au kuuza bidhaa nje ya nchi.
Mkurugenzi mkuu wa chama cha wasafirishaji shehena cha Afrika Mashariki SCEA Bw. Gilbert Langat amesema, kwa kawaida wafanyabiashara wanapoteza asilimia 2 ya mizigo yote inayosafirishwa kupitia barabara kuu kati ya Mombasa na Nairobi.
Bw. Langat amesema hayo kando ya uzinduzi wa sera za kipaumbele za chama cha wazalishaji cha Kenya, huku akiongeza kuwa reli ya SGR inatarajiwa kuondoa hasara za mizigo kutokana na reli hiyo kuwa na usalama mkubwa wa mizigo.
Wafanyabiashara ambao wanatumia barabara kuu hupoteza mizigo kutokana na wahalifu wanaoibia mizigo wakati malori yameegeshwa vituoni katika barabara kuu kutoka Nairobi hadi Mombasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |