• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa mapendekezo kuhusu mageuzi ya mfumo wa maendeleo ya Umoja huo

    (GMT+08:00) 2017-07-06 16:47:24

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa mapendekezo kuhusu mageuzi ya mfumo wa maendeleo wa Umoja huo ili kuihimiza jumuiya ya mataifa kutekeleza ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030.

    Bw. Guterres amesema mfumo wa maendeleo wa Umoja huo umetunga hatua nyingi za kuwasaidia watu maskini na dhaifu duniani kuboresha maisha yao, lakini bado unahitaji kukamilishwa katika mchakato wa kufuata ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 kutoka Malengo ya Maendeleo ya Milenia.

    Katibu mkuu huyo ametoa kanuni 8 za uongozi kwenye mapendekezo yake, zikiwemo Umoja wa Mataifa kutoa mapendekezo na ustadi wa kitaaluma, na kuzisaidia nchi mbalimbali kutimiza malengo ya maendeleo endelevu katika pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako