• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la mashariki nchini Libya latangaza kudhibiti mkoa wa Benghazi

    (GMT+08:00) 2017-07-06 16:50:26

    Kamanda wa jeshi la taifa la Libya lililoko mashariki mwa nchi hiyo Meja Jenerali Khalifa Haftar ametangaza kuwa vikosi vyake vimefanikiwa kushinda makundi pinzani ya wapiganaji na kudhibiti mkoa wa Benghazi baada ya mapigano yaliyodumu kwa miaka mitatu.

    Vikosi vya Haftar, vikishirikiana na mamlaka za mashariki mwa Libya, vilikuwa kwenye mapigano makali kwa miaka mitatu dhidi ya makundi ya wapiganaji katika mkoa huo ambao ulikuwa ngome kuu ya waasi.

    Meja Jenerali Haftar amesema, katika tukio hilo la kihistoria ambalo wananchi wa Libya wamelisubiri kwa muda mrefu, jeshi la Libya linapenda kuwashukuru askari wake shupavu, na kuzishukuru nchi rafiki zilizoliunga mkono.

    Libya bado inakabiliwa na machafuko na mgawanyiko wa kisiasa, licha ya kusaini makubaliano ya amani chini ya Umoja wa Mataifa na kuanzishwa kwa serikali ya umoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako