• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Chama cha wafanya biashara Kampala chaahirisha maandamano

    (GMT+08:00) 2017-07-06 17:38:03

    Chama cha wafanya biashara mjini Kampala nchini Uganda (Kacita) kimeahirisha maandamano waliokuwa wanapanga kushinikiza spika wa bunge kuwa sheria mpya ya kuthibitikodi za nyumba.

    Juni 15 Kacita ilimuomba spika wa bunge Rebecca Kadaga kuharakisha mpango wa kuwa na sheria hiyo.

    Hata hivyo sasa spika huyo ameitaka serikali kuharakisha mchakato ili wafanyabiashara waanza kufurahia manufaa yake.

    Mwenye kiti wa Kacita Everest Kayondo, amesema wafanyabiashara wametaka kuwa na sheria hiyo mpya ili kuwalinda dhidi ya wenye nyumba ambao wanalipisha fedha nyingi za kawi.

    Spika Kadaga amewaandikia barua wafanyabiashara akiwahakikishia kuwa bunge linajadili na serikali na pia wizara husika ili kutayarisha mswada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako