• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Uchumi wa Rwanda wakua kwa franc bilioni 224 robo ya kwanza ya 2017

    (GMT+08:00) 2017-07-06 17:38:32

    Uchumi wa Rwanda umekua kwa franc bilioni 224 katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ukisaidiwa na sekta ya utoaji huduma.

    Kulingana na taasisi ya kitaifa ya takwimu (NISR) pato la taifa sasa limefikia franc bilioni 1,817 billion, kutoka bilioni 1,593 kipindi sawa na hicho mwaka 2016.

    Mkurungezi wa taasisi hiyo Yusuf Murangwa, amesema ukuaji kwenye sekta ya utoaji huduma imechangiwa na utendaji mzuri wa hoteli ambayo ilikuwa kwa asilimi 17.

    Kwa jumla sekta ya huduma imekua kwaasilimia 4 na hivyo kuchangia ukuaji wa asilimia 46 wa uchumi wa taifa.

    Sekta nyingine ambazo zimechagia ukuaji ni kilimo na utengenezaji bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako