• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Rais wa Zanzibar asema bei ya karafuu haitashuka

    (GMT+08:00) 2017-07-06 17:39:39

    Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali haijaona sababu ya kushusha bei ya ununuzi wa karafuu kutokana na wakulima kuimarisha kilimo cha zao hilo.

    Dk Shein amesema hayo akizungumza na uongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) na watendaji wa ofisi hizo Ikulu mjini Zanzibar.

    Amesema jitihada za wakulima zinatokana na mageuzi yaliyofanywa na Serikali katika kipindi cha miaka sita iliyopita kuanzia 2011, kwa kupandishwa bei ya karafuu kwa wakulima kutoka Sh5,000 hadi Sh14,000 kwa kilo moja.

    Aidha ameahidi Serikali itazidi kuunga mkono jitihada za wakulima kwa kadri hali itakavyoruhusu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako